Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children

Shughuli Zitakazofanyika

  1. Siku ya kwanza tarehe 26/11/2018 – kutafanyika tendo la Kijamii katika Halmashauri ya Jiji la Arusha katika Kituo cha Afya Kaloleni ambacho kipo katikati ya mji jirani na mnara wa Mwenge hapo kuna makumbusho ya Azimio la Arusha. Pia watakabidhi vifaa tiba Mgeni rasmi wa tukio hili la kijamii atakuwa Katibu Mkuu - MJW.
  2. Siku ya pili na ya tatu tarehe 27–28/11/2018, kutafanyika Kongamano la Watalaam katika ukumbi wa Lush Garden Hotel. Aidha, siku hiyo hiyo tarehe 27/11/2018 kutafanyika uzinduzi wa Maktaba ya Taasisi ya Tengeru. Wakati wa kongamano yatakuwepo maonesho ya kazi zinazotekelezwa na maafisa Maendeleo ya Jamii yatakayohusisha Wizara, Taasisi, Mamlaka za Serikali, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Vyuo na Taasisi za Elimu. Mgeni rasmi wa matukio haya mawili Kuzindua Maktaba na Kongamano atakuwa Mhe Jenista Mhagama (MB).

    Aidha, Kongamano litafungwa tarehe 28 Novemba, 2018 na Mgeni Rasmi atakuwa Mhe Ummy Mwalimu (Mb) –WAMJJW. Tukio muhimu litakaloambatana na kufunga kongamano ni uzinduzi wa Mwongozo wa WDF uliofanyiwa mapitio na Mwongozo wa Uhamasishaji Wanawake kuanzisha na kujiunga na vikundi vya kiuchumi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Pia Mgeni rasmi atatoa tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri katika kuchangia asilimia tano (kwa sasa 4) kwa ajili ya mikopo ya wanawake na Vyeti kwa washiriki walioandaa Mtaala wa Vyuo vya CDTIs na CDTTIs .

  3. Huduma za Afya (upimaji VVU na Magonjwa yasiyoambukiza zitatolewa wakati wote wa kipindi cha Kongamano na Mkutano); na
  4. Siku ya mwisho tarehe 29/11/2018 kutafanyika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) na utaongozwa na rais wa chama.