Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children
Na. Name DAy Action
1 Ukatili wa Kijinsia Day one Download
2 Majukumu ya Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Day one Download
3 Usimamizi na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo Day one Download
4 Umuhimu wa Taaluma ya Maendeleo ya Jamii Day one Download
5 Mabadiliko ya Fikra na Mtazamo Day Two Download
6 Umuhimu wa Tafiti Day Two Download
7 Mchango na Uzoefu wa Sekta Binafsi Day Two Download
8 Mchango na Uzoefu wa Sekta Binafsi Day Three Download

Mada

Mada Kuu jumla yake ni 4; Mada hizo na wawasilishaji ni kama ifuatavyo:-

 1. Katibu Mkuu- MJW- Majukumu ya Wataalamu wa Maendeleo ya Katika Sekretariati za Mikoa na Mamlaka za serikali za Mitaa.
 2. Prof. S. Wangwe- atawasilisha mada ya Umuhimu wa Taaluma ya Maendeleo ya Jamii katika Kuelekea Uchumi wa Kati 2025. Mjadili mada atakuwa Bahati Rukiko kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
 3. Prof. John F. Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA)- atawasilisha mada ya Uzoefu na Changamoto katika Usimamizi na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo- Mjadili mada hii atakuwa Bi. Janet Zemba Mhadhiri kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.
 4. Dkt Katanta Simwanza kutoka Plan Tanzania –atawasilisha mada ya Ukatili wa Kijinsia, Ukeketaji, Ndoa na Mimba za Utotoni vinavyoathiri jamii katika kuelekea Uchumi wa Kati, 2025. Mjadili mada hii atakuwa Dkt. Magreth Msonganzila- Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi

Aidha, Kutakuwepo na Majadiliano Kivikundi (Parallel sessions) yatafanyika kwa siku ya pili ya mkutano ambapo washiriki watagawanyika katika makundi matatu na mada kwa kila kundi ni kama ifuatavyo:-

 1. Kundi Na. 1: Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka RS na MSM

  Mada mbili zitawasilishwa Mabadiliko ya Ki fikra na Mtazamo katika Utekelezaji wa Majukumu ya Maafisa ya Maendeleo ya Jamii. Mtoa mada atakuwa Dk. Chris Mauki, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

  • Vilevile kwa kuzingatia kuwa washiriki wa kundi hili ni Wasajili Wasaidizi wa NGO’s, itawasilishwa mada ya mahsusi kwa ajili yao Usajili na Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa Wasajili Wasaidizi itakayowasilishwa na Katibu Mkuu - WAMJJW na pia Majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kukuza ajira – itakayowasilishwa na OR TAMISEMI
 2. Kundi Na. 2: Watalaam wa Maendeleo ya Jamii kutoka sekta Binafsi

  Mada itakayowasilishwa ni Mchango na Uzoefu wa Sekta Binafsi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Kutekeleza Shughuli za Maendeleo ya Jamii. Mtoa mada atakuwa Ndg. Hamisi Mkomwa kutoka Shirika la Small Enterprises Institutional Development Associate (SEIDA).

 3. Kundi Na. 3: Waadhihiri na Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya jamii.

  Mada itakayowasilishwa ni Umuhimu wa Tafiti katika Utatuzi wa Changamoto za Jamii. Mtoa mada atakuwa Ndg. John Gwanyemba na Bi. Janet Zemba wahadhiri kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru